hii ilikuwa ni moja kati ya maonyesho makubwa ya nguo duniani jijini milan(ITALY) toka kwa mbunifu mkubwa,TOMMY HILFIGER,'maonyesho ambayo yalifaana sana,wabunifu wa kitanzania mnatakiwa muige mifano mizuri kama hii kwa ubunifu wa hali ya juu na kutoa nafasi pia kwa wanamitindo wote wale ambao wanastahili na wenye sifa hasa zinazotakiwa kwenye mitindo,sio unachukua mtu kwa sababu unajuana naye ama kwa kukimbia kumlipa kiwango cha malipo kinachostahili,hii itakuwa inaangusha fani yetu na kuwavunja moyo wanamitindo wetu wakitanzania wenye kuipenda fani hii lengo ni kusonga mbele na sio kurudi nyuma kwa pamoja tushirikiane kuinua fani yetu ambayo iko ukingoni.."one love" |
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!